Snura
Mushi ambaye ni star wa filamu na muziki nchini amezua habari mpya ya
kudaiwa kuwa muumini mzuri wa waganga wa kienyeji a.k.a Sangoma. Kwa
mujibu wa Bossngasa blog chanzo kimoja kiliutonya mtandao huo kuwa Snura
ana mambo hayo ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kila mara.
Baada
ya kuzipata habari hizo mtandao huo uliweka mtego kwa Snura na ukanasa
baada ya kumuona akiwa amevalia tofauti huku mtu mwingine ikiwa si
rahisi kumtambua kuwa ni Snura Star wa wimbo wa Majanga. Snura aliingia
kwa mganga huyo akiwa amebeba jogoo jekundu na kufanyiwa ndumba kwa
mujibu wa mtandao huo.
Snura
No comments:
Post a Comment