Friday, 3 January 2014

DIAMOND AUSIFIA UZURI WA WEMA SEPETU BAADA YA KUACHA MKOROGO, ATAKA WAZAE MTOTO.

Diamond Platinumz ameonekana kuvutiwa na ngozi ya mpenzi wake Wema Sepetu baada ya kuacha kutumia mkorogo ambao ulikuwa tayari umeshaanza kumharibu ngozi yake na kupelekea kwenda nchini China kufanyiwa marekebisho ya ngozi na kupewa ushauri wa kitaalaam ikiwemo kutotumia tena mkorogo au madawa ya kujichubua kwani ni hatari kwa ngozi na afya ya binadamu. Akizungumza na gazeti moja Diamond alisema "Umemwona Wema, kwa sasa ana ngozi nzuri yenye afya na iliyo na mng’aro kama alivyokuwa awali,ni nzuri sana yani,  ameacha kabisa kutumia dawa za kung’arisha ngozi hilo ndilo lililonivutia zaidi kwani alisikiliza ushauri niliompa kabla"

 Star huyo wa nyimbo za My Number One, Mbagala na Kamwambie aliendelea kwa kusema kuwa Wema ndiyo chaguo lake na nia yake ya kuzaa nae mtoto iko palepale "Miezi kadhaa nyuma niliongea kuhusu nia yangu ya kuzaa na Wema, wakati huo nilikuwa bado na Penny, siwezi kukimbia kivuli changu kwani ukweli unabaki palepale nampenda yule binti, japokuwa wapo wanaosema kwamba sijatulia au natafuta ‘kiki’ kupitia warembo hawa, si kweli, Wema nilikuwa naye kabla ya Penny na vigezo vyangu ni mchumba anayejali kazi yangu na kujua kwamba mimi ni staa nahitajika sehemu yoyote, muda wowote, Wema ni mwelewa"







credit: swahiliworldplanet
                                     Wema Sepetu na Diamond


No comments:

Post a Comment