Thursday, 23 January 2014

LULU APATA MCHUMBA, KUOLEWA MUDA SI MREFU !

Elizabeth Michael(Lulu) ambaye ni star mkubwa wa filamu Swahiliwood anadaiwa kuwa na mchumba ambaye anajulikana kwao tayari. Mchumba wa Lulu anadaiwa kuwa kigogo mwenye pesa zake na pia mmiliki wa kampuni moja kubwa ya usambazaji wa filamu na anajulikana kwa jina la Johnson au Jr. Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kilisema .......



"Kwa taarifa yenu, tayari JR anafahamika vizuri kwa akina Lulu kwani alishakwenda kujitambulisha na kuna maneno kwamba ndiye aliyempangia nyumba kubwa, Tegeta jijini Dar. Unajua yule jamaa aliona fursa akaitumia baada ya Lulu kutoka mahabusu kwa matatizo ya kifo cha mwandani wake, Steven Kanumba ndipo JR akafanya juu chini hadi akafanikiwa"

Chanzo hicho kiliendelea kwa kusema "Muda si mrefu zitasikika cherekochereko za Lulu kuolewa. ukweli nin kwamba hata mama Lulu(Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo sasa, sasa hivi Lulu anaishi kwenye bonge la nyumba kule Tegeta(Dar es salaam) na suala la usafiri si ishu, Anabadili tu magari, kusema kweli kwa sasa bidada mambo yamemwendea vizuri, Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu"

Naye mama Lulu alipoulizwa na mtandao huo kuhusu issue hiyo alisema kuwa yeye hana kipingamizi kwakuwa hayo ni maelewano ya Lulu na mchumba wake na anamkubali mchumba huyo na alipoulizwa kuwa mwanaume huyo ni kigogo mwenye fedha zake alisema "mimi sina sababu ya kumkataa mwanaume ambaye wamekubaliana na mwanangu, kikubwa ni makubaliano, namkubali"

Lulu alipotafutwa mazungumzo yake na mtandao huo kupitia gazeti lake la Amani yalikuwa hivi.........

Amani: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa, naongea na nani?
Amani: (akatajiwa jina la mwandishi) kwanza hongera kwa kupata mchumba.
Lulu: Nani kawaambia?
Amani: Kwa kazi yetu hii hatushindwi kujua. Je, ni kweli umepata mchumba?
Lulu: Ndiyo lakini nisingependa sana kulizungumzia hilo.
Amani: Anaitwa nani?
Lulu: Siwezi kumtaja leo (Jumanne iliyopita). Nitawatajia tu ninyi subirini. Itakuwa surprise (mshangao), siku si nyingi nitamuanika.
Amani: Je, ni kweli ni maarufu kwa jina la JR? Au wewe tutajie hata jina la mwanzo tu.
Lulu: Nimeshasema jamani nitawatajia kwani ninyi mna haraka gani?
Amani: Je, ni kweli ni mmiliki wa kampuni ya burudani? (anatajiwa kampuni).
Lulu: Hayo yote yatafahamika kwenye utambulisho. Naomba niishie hapo ‘coz’ sina cha zaidi kuhusu ishu hiyo jamani subirini siku si nyingi.


Naye Flora Mtegoa ambaye ni mama wa Kanumba alipogusiwa kuhusu Lulu kupata mchumba alionyesha kuchekelea na kusema hana tatizo kabisa kwani Lulu tayari ni mtu mzima.
"Mimi sina tatizo kabisa, namjua. Lulu anaweza kuolewa na nimempa baraka zote" alisema mama Kanumba ambaye kwa sasa ni shosti mkubwa wa mama Lulu.

Kwa upande  wa JR alipotafutwa na mtandao huo ilikuwa hivi..

Amani: Habari yako mkuu JR?
JR: Safi, nikusaidie nini?
Amani: Mimi…(akatajiwa jina la mwandishi na kampuni) wewe ndiye JR mmiliki wa kampuni ya…(anatajiwa jina la kampuni).
JR: Kwanza mimi siyo JR ni GR. Huyo JR ni mdogo wangu.
Amani: Mbona sisi tumetajiwa JR ambaye anamiliki kampuni ya...(anatajiwa tena jina la kampuni).
JR: Oke, ndiyo mimi nikusaidie nini?
Amani: Taarifa tulizonazo ni kwamba una uhusiano na Lulu? Yaani wewe ndiye mchumba wake?
JR: Ndiyo, sitaki maswali (tusi na kukata simu).
Tangu kitokee kifo cha Kanumba ambaye alikuwa na uhusiano wa siri na Lulu, bidada huyo hajawahi kuwa na mwanaume hadi huyo mchumba aliyejitokeza.

                                                  Lulu

No comments:

Post a Comment