Thursday, 23 January 2014

LULU NA STEVE NYERERE KUONEKANA THE MBONI SHOW LEO ALHAMISI.

 Msanii wa Maigizo Tanzania Steve Mongere aka Steve Nyerere akisalimiana na Mwendesha Kipindi cha The Mboni Show , Mboni Masimba (Wa Kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili ndani ya mjengo ambapo kipindi hiko hurekodiwa Pembeni ni Msanii nguli wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael "Lulu" akifuatiwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa Filamu za Kitanzania Nchini.

Msanii Nguli na mahiri aliye chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited Elizabeth Michael "Lulu" akisikiliza kwa makini wakati msanii mwenzie Steve Nyerere alipokuwa akiongea katika kipindi cha The Mboni Show
 Mwendeshaji wa Kipindi cha The Mboni Show Mboni Masimba (Wa Kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Muigiza Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu aliye chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited mara baada ya kipindi kumalizika
 Meneja masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Evance Steven akiwa tayari kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Mwendesha Kipindi Cha The Mboni Show, Mboni Masimba wakati wa kurekodi kipindi hiko kitakachorushwa leo Alhamisi
 Muigiza wa filamu za vichekesho Steve Mogere "Nyerere" akieleza mikakati yake na filamu zake mpya alizotoa akiwa chini ya Kampuni ya Utengenezaji, Usambazaji na Uuzaji wa Filamu za Kitanzania ya Proin Promotions Limited wakati wa kipindi cha the Mboni Show kitakachorushwa hewani leo
 Mboni Masimba, mwendeshaji wa Kipindi cha the Mboni Show akimsikiliza Steve Nyerere kwa umakini wakati msanii huyo wa vichekesho alipokuwa akielezea Mikakati yake katika Mwaka huu na juu ya filamu zake alizozitoa akiwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited 
 Mwendeshaji wa kipindi cha the Mboni Show, Mboni Masimba (wa kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni aliowaalika katika kipindi chake cha The Mboni Show kitakachorushwa leo usiku. Kutoka Kulia Ni Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Evance Stephen, Msanii Nguli na Mahiri Elizabeth Michael aka Lulu na Steve Mongere aka Steve Nyerere.

No comments:

Post a Comment