Star wa filamu Swahiliwood Salma Jabu Nisha ameonekana kukerwa na baadhi
ya magazeti na mitandao iliyoandika kuwa ametoa mimba juzi kati wakati
alipokuwa akiumwa na kukimbizwa hospitali. Hata hivyo Nisha alikuwa
akiumwa sana kichwa kitu ambacho mwenyewe kimemshangaza kutokana na
wanaozusha kuwa ametoa mimba. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Star huyo
wa filamu za Tikisa, Boss Tony, Pusi Na Paku na Matilda aliandika
........
"Sipendi ujinga usokuwa naa akili,kama mmekosa cha kuandika nendeni
vijijini kuna watu kibao wanapata shida na kodi zetu zinaliwa na waroho
wa mali za wananchi,kuna wanaokufa kila siku kwa kukosa huduma za msingi
km hospital,chakula n.k,naamini kwa kuandika kwenu basi nchi yetu
itapata faida angalau,siyo unakurupuka mimi.naumwa kichwa unaandika
NIMETOA MIMBA.. je hiyo mimba kanipa baba yako?? Au wakati natoa
ulinisindikiza? Mimi.ni muislam dhahir na najua madhara ya kuua kiumbe..
so ww ulieandika ujinga huo,rudi shule na ujifunze kanuni za uandishi
Samahanini sana mashabiki zangu kwa mlokutana na hili,si wote wanaotembea mabarabarani ni wazima,"
No comments:
Post a Comment