Shilole ambaye ni star wa filamu na muziki nchini Tanzania amenasa
kwenye penzi la jamaa wa kizungu raia wa Uingereza anayejulikana kwa
jina la Ankar. Jamaa huyo kwa mara ya kwanza alidatishwa na shilole
katika show aliyoifanya nchini Uingereza. Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kilisema "Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye
shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi
karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake"
Naye Shilole alipoulizwa na mtandao huo alisema " Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa
napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu
yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda
ndipo tukaanzisha urafiki, Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum
alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita
nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole"
Shilole na mpenzi wake huyo
No comments:
Post a Comment