Sunday, 19 January 2014

DIVA KUGOMBEA UBUNGE UCHAGUZI MKUU 2015.

Diva
Loveness Malinzi a.k.a Diva ambaye ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Ala Za Roho kinachorushwa na Clouds fm ametangaza nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Diva ameandika maneno hayo hapo chini katika mtandao mmoja wa kijamii.

 Hata hivyo inadaiwa kama Diva atagombea ubunge anaweza kupata support ndogo kutoka kwa wanawake wenzake ambao ni moja ya kundi linalodaiwa kuwa mstari wa mbele kupiga kura kipindi cha uchaguzi kwani inadaiwa ni mtu wa kujishaua na kujikomba sana hivyo anaweza asifanikishe azma yake hiyo kama asipojipanga vizuri kama mwanasiasa kwani siasa si lelemama. Star mmoja wa filamu nchini baada ya kuona alichoandika Diva aliuambia mtandao huu kwa kusema  "Diva ni mtu wa kujishaua na kujikomba sana atakuwa na wakati mgumu kupata sapoti kutoka kwa sisi wanawake wenzake kwani namjua vizuri sana, anatakiwa ajue kuwa siasa sio sehemu ya mashauzi kama utangazaji, siasa ni kuwatumikia wananchi ndio tutamuunga mkono akija kupata huo ubunge mjini hapatalalika nakwambia" alisema star huyo wa filamu ambaye amedai kujuana vizuri na Diva.


 Hivi majuzi imedaiwa Diva na watangazaji wenzake B12, Adam Mchomvu, na Dj Fetty wamesimamishwa kazi Clouds fm kwa utovu wa nidhamu.

 Mtangazaji huyo mwenye sauti tamu ameandika hivi..........

kila la kheri Diva................

No comments:

Post a Comment