Monday, 27 January 2014

PETER PHINIAS KUCHEZA FILAMU YA MAISHA HALISI YA KANUMBA !

Peter Phinias
Hivi karibuni mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba alisema kuwa ana lengo la kutengeneza filamu itakayohusu maisha halisi ya mwanae marehemu Steven Kanumba ambaye alikuwa star mkubwa wa filamu nchini aliyekuwa tayari ameanza kukubalika katika nchi kadhaa za kiafrika ikiwemo Nigeria kwa juhudi zake alizozifanya kupitia filamu na kufanikiwa kuanza kuitangaza Tanzania vizuri. mama Kanumba ambaye jina lake halisi ni Flora Mtegoa alisema kuwa atafanya usaili wa kutafuta muigizaji wa kiume anayefanana na Kanumba ili acheze nafasi ya maisha ya Kanumba, na hataangalia umaarufu wa mtu bali kipaji na kufanana na Kanumba.

Steven Kanumba

Kama hiyo ikitokea basi Peter Phinias ambaye ni muigizaji chipukizi nchini anayedaiwa kufanana na Kanumba anaweza kupata nafasi ya kuigiza filamu hiyo, Peter Phinias tayari ameigiza kwenye filamu ya Mahaba Niue akiwa na Jackline Wolper na Simon Mwapagata(Rado) na Mistake Vision akiwa na Deogratiaus Shija. Ukiachilia mbali Phinias muigizaji mwingine wa filamu anayedaiwa kufanana na Kanumba ni Philimon Lutwaza ambaye tayari ameshaigiza filamu kadhaa na mastaa wengi nchini ikiwemo After Death amabyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba.

Wiki mbili zilizopita baadhi ya mitandao kadhaa nchini na hata page ya East Africa Television iliweka picha ya Peter Phinias kuwa anafanana na Kanumba na kuwataka watu wampe asilimia za ufanano wake na Kanumba. Je wewe unadhani Peter anafanana na marehemu Kanumba kwa asilimia ngapi?

A. 100%

B. 85%

C. 70%

D. 50%

E. 0%
                                                              Peter Phinias

No comments:

Post a Comment