Muigizaji maarufu wa filamu nchini Blandina Chagula(Johari) anadaiwa
kuwa amelazwa katika hospitali moja jijini Dar es salaam kutokana na
kuumwa ingawa bado haijajulikana nini kinamsumbua star huyo mkongwe wa
filamu Swahiliwood. kwa mujibu wa mtandao mmoja ndugu mmoja wa Johari
alisema kuwa Johari anaumwa sana na amelazwa hospitali moja jijini Dar
es salaam lakini alikataa kuitaja hospitali hiyo kwa kuhofia waandishi
wa habari akidai watamsumbua star huyo "kwa kweli Johari anaumwa sana na
tunaomba dua zenu tu" alisema ndugu huyo.
Ugua pole Johari
No comments:
Post a Comment