Muigizaji wa filamu nchini Yuster Nyakachaka ambaye filamu yake mpya
akiwa na Jackline Wolper na Slim Omar inatarajiwa kutoka muda si mrefu
ametoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha watoto yatima na kina
mama wajane wasiojiweza. Yuster muigizaji mwenye muonekano na umbo la
kistaa alitembelea kituo hicho kitwaacho Madale Orphanage Centre
kilichopo madale kata ya wazo. Muigizaji huyo aliandaa chakula cha
mchana katika kituo hicho na pia kutoa vyandarau 400 kwa watoto na kina
mama wajane waishio katika kituo hicho kama picha zinavyoonekana hapo
chini. Muigizaji huyo pia alitoa vitu vidogo vidogo kama vile sabuni,
mafuta ya kujipaka, nguo na viatu kwa watoto wote na pia khanga na
vitenge. Angalia picha hapo chini.
Yuster aliyeshika mtoto akiwa na kina mama wa kituo hicho jana
Yuster akitoa msaada wa vitu mbalimbali jana katika kituo hicho
Wasanii wengine mliondekeza starehe bila kurudisha chochote kwa jamii inayosapoti kazi zenu igeni mfano.
Mungu akuzidishie sana Yuster kwa kuonyesha moyo wa kusaidia walio katika mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment